FAQs – Swahili

FAQs – Swahili

FAQs

Maswali Yanayoulizwa Sana

 • Premise inafanya nini?

  Premise hufanya aina mbalimbali za tafiti ili kutathmini hali ya maisha ya jamii kutoka kila kona ya dunia kusaidia mashirika kujibu maswali yao muhimu. Changia ufahamu wako juu ya jamii yako kwa kukamilisha task rahisi, kama vile kutoa maoni, kukamilisha dodoso fupi au kupiga picha ndani ya mji wako kusaidia mashirika kufanya maamuzi sahihi na yanayofaa.

 • Premise inafanya kazi na nani?

  Premise inafanya kazi na serikali za nchi tofauti, mashirika ya misaada, na makampuni. Wateja wetu wa sasa na wa zamani ni pamoja na Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani, pamoja na Benki ya Dunia.

 • Ninawezaje kuwa Mchangiaji?

  Unachohitaji ni simu janja pamoja na app ya Premise, ambayo unaweza kuipakua kutoka Duka la Google Play au Apple App Store. Pakua app, tengeneza akaunti na kamilisha task za kwanza kuanza kujipatia fedha.

 • Premise inapatikana wapi?

  Kwa sasa tunafanya kazi ndani ya nchi zaidi ya 70, katika kila kona ya dunia na tunaenea kwa kasi. Task zinapatikana kulingana na mahitaji ya mashirika tunayofanya nayo kazi, kwahiyo upatikanaji unaweza kubadilika mara kwa mara.

 • Je, nitahitaji aina flani ya simu?

  Kutegemeana na eneo, app ya Premise inaweza kupatikana kwenye Duka la Google Play na Apple App Store. Hata hivyo, app inapatikana kwenye vifaa vya Android ndani ya maeneo fulani. Na simu ya Android inatakiwa kuwa na toleo la 4.0 au zaidi ili app iweze kufanya kazi.

 • Je, ninahitaji kuwa nimeunganishwa kwenye mtandao wa intaneti au Wifi?

  Ndiyo, mtandao wa intaneti unahitajika ili kuweza kupata tasks, kuzikamilisha na kutuma maombi ya kutoa malipo.

 • Ninaweza kupata kiasi gani cha pesa kutoka Premise?

  Kiasi cha pesa ambacho Wachangiaji wanaweza kukipata hutegemea na idadi ya tasks walizokamilisha. Baadhi ya wachangiaji wetu wanatumia mapato yao kulipa ada za shule, kuchangia watu wasio na makazi kupata chakula, na kukamilisha ujenzi wa nyumba. Tunatumia njia tofauti za malipo, kama vile Coinbase, Paypal na Mobile Money kurahisisha malipo.

 • Kuna kikomo cha idadi ya task ninazoweza kukamilisha?

  Kikomo kilichopo kwenye uwezo wako wa kukamilisha task hutegemea uhitaji wa taarifa kuhusiana na eneo na idadi ya wachangiaji wengine karibu yako wanaohifadhi task kwa ajili ya kuzifanya. Kukamilisha task nyingi iwezekanavyo, tunapendekeza uangalie soko la kazi ndani ya app mara kwa mara, kuhifadhi task unayotaka kuifanya, na kuikamilsha mapema iwezekanavyo kabla haijahifadhiwa na mwingine.

 • Premise ni salama?

  Premise daima tumejikita kwenye usalama na ustawi wa Wachangiaji wetu na tunafanya kazi kuhakikisha wanapata furaha kila wanapotumia app yetu.Tunachukua hatua tofauti za kuhakikisha usalama, kama vile kufanya kazi na Wataalamu wetu wa Msaada wa Nchi (Country Support Specialists) kubuni tasks na kupata ufahamu na uelewa wa ndani juu maeneo tunayofanya kazi. Habari za kibinafsi zinatumika kuhakikisha ubora wa taarifa na kusadifisha mtandao — ambapo habari hizi zakuhusu, zimefichwa (encrypted) kulinda faragha yako.

 • Ninahitaji kuwasha upatikanaji wa kitambua eneo na kamera?

  Task zetu mara nyingi zinakuhitaji kupiga picha au kwenda katika maeneo fulani, ndio sababu tunayohitaji upatikanaji wa ruhusa kama vile kitambua eneo (mahali) na kamera kuwa zimewashwa.

Kama una maswali ya ziada, tafadhali tutumie barua pepe kwenda support@premise.com.

Start making money now.

Android app on Google Play